RC Iringa Dr Christine Ishengoma
NA FRANCIS GODWIN BLOG
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma ametuma salama kali za Krismas na Mwaka mpya kwa wafanyabiashara watakaopandisha bei ya vyakula msimu huu wa sikukuu kuwa watachukulia hatua kali.
Huku akiwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya ,wakuu wa wilaya ,maofisa biashara wa wilaya na mkoa huo kuanza kuzunguka mitaani kuchunguza bei ya bidhaa na kuwataka kuchukua hatua kwa wote wanaliopandisha bei kiholela.
Akizungumza na wanahabari jana ofisini kwake ,mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia sikukuu mbali mbali kujipatia fedha kwa kuwanyonya wananchi jambo ambalo katika mkoa huo halitavumiliwa kamwe.
Alisema kuwa lengo la serikali ya mkoa kuwabana wafanyabiashara ni kutaka kuona wananchi wanasherekea sikukuu hizo na kununua vyakula na vitu mbali mbali vya sikukuu kulingana na bejeti waliyoitenga kwa sikukuu hizo.
” Serikali ya mkoa haitakubali kuona wananchi wakiibiwa kwa kuuziwa vyakula kwa bei kubwa za sikukuu….tumejipanga kuchukua hatua kali na tunaomba wananchi pia kutoa ushirikiano “
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alivipongeza vyomba vya habari mkoani Iringa kwa mchango mkubwa wa kuhamasisha maendeleo na kutaka kuonyesha ushirikiano katika wakati huu wa sikukuu kwa kufanya uchunguzi wa wafanyabiashara wanaopandisha bei.
Katika hatu nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbali mbali yakiwemo yale yanayohimili ukame kwa maeneo yeye changamoto ya mvua.
Pia aliwataka maofisi kilimo na mabwana shamba kuachana na mpango wa kuvaa suti na kushinda maofisini wakati huu wa msimu wa kilimo badala ya kwenda kuwaelimisha wakulima .
Dr Ishengoma aliwataka wakulima kuendelea kutumia mbolea ya Minjingu ambayo alidai hata yeye amekuwa akiitumia na ni miongoni mwa mbolea bora nchini na kuwataka kuepuka maneno ya kukatisha tamaa yanayoendelea kutolewa na watu juu ya mbolea hiyo.
Wakati huo huo serikali ya mkoa wa Iringa imepiga marufuku wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda kushiriki madisco toto ambayo alidai ni hatari na ni vema wazazi na walezi wa watoto mkoani Iringa kuwa makini na kuachana na tabia ya kuwaacha watoto wao peke yao wakati huu wa sikukuu.