
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO ENEO LA KUEGESHA MAGARI YA KAMPUNI YA SUNSHINE MINING LTD KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA
YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MSABAHA S/O RASHID KAFULAMA, FUNDI MKUU WA KUTENGENEZA MAGARI WA KAMPUNI HIYO ALIIBA GARI T.421 CHG AINA YA TOYOTA L/CRUISER SINGLE CABIN RANGI NYEUPE CHASES NO JCLB-715407036705 LENYE THAMANI YA USD 35,000 NA KWENDA MAHALI KUSIKOJULIKANA. MBINU NI KUJARIBU KUENDESHA GARI HILO BAADA YA KULIFANYIA MATENGENEZO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA PAMOJA NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA MOTO.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:15HRS HUKO KATIKA SHULE YA WASICHANA YA SEKONDARI IGUMBILO INAYOMILIKIWA NA KANISA LA LUTHERANI, ILIYOPO KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. BWENI MOJA LA SHULE HIYO LILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA BWENI HILO. CHANZO BADO KUFAHAMIKA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI HITILAFU YA UMEME. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO].
[GONGO].
MNAMO TAREHE 07.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:50HRS HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI CHA MPONZI KILICHOPO KATA YA KAGERA, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA /MSAKO WALIMKAMATA PRISCA D/O GODWIN, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA KAGERA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1.5. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI - SACP].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.