Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

AJALI YA GARI LILILOKUWA LIMEBEBA MAZAO YA KITUNGUU NYANZWA HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA.

$
0
0
Gari aina ya Dyana likiwa nimelele barababi mwishoni mwa wiki muda mfupi tu baada ya kupinduka.

Wananchi wa kijiji cha Igunda waliwa katika harakati za kushusha magunia ya vitunguu katika gari lilipinduka katika eneo hilo.








Majeruhi katika ajali hiyo ambao baadhi yao hawakujulikana majina yao mara moja


Majeruhi jamii ya kimang`ati wakiuugulia machungu ya maumivu baada ya kupata ajali hivi karibuni katika kijiji cha Igunda wilayani kilolo-Iringa.waliomba liti katika gari la mizigo,lakini hakuna mtu hata mmoja aliyepoteza maisha.


Kijana Wasafiri Kibulla Ambaye pia ndiye dereva wa gari hilo akiwa amepakatwa na mama yake mzazi kufuatia maumivu aliyoyapata katika ajali hiyo.


Dereva wasafiri Kibulla akiw ameshikiliwa na mama yake mzazi.




Jeraha la kijana wa kimang`ati baada ya kuumia katika ajali hiyo.



Aliumia pia katika mbavu zake baada ya ajali hiyo.

HABARI KWA UNDANI;
 Ilikuwa siku ya jumamosi mchana muda mfupi tu baada ya mkutano wa mkuu wa wilaya ya Kilolo na wataalam wa mswala ya mazingira na kilimo wapokutana kuzungumzia swala la kukauka kwa mto ruaha katika vijiji vya Nyanzwa na Igunda,ndipo ambapo gali lenye nambari za usaji T343 ARY Dyana lililokuwa limesimama kwa muda mrefu kabla ya msafara wa kuu huyo wa wilaya kuondoka likaanza safari yake ya kuelekea mtandika ambako lilikuwa likipeleka zao hilo la kitunguu.

Gari hilo lilipinduka kufuatia kuelemewa na ubovu wa barabara hiyo ambayo kwa mujibu wa wahanga wa ajali hiyo walisema kuwa gari ilikosa mwelekeo baada kufuatia ufinyu wa barabara hiyo iliyojengwa na halmashauri ya wilaya ya kilolo.

Wakizungumza na mtandao huu wananchi hao walisema barabara ni finyu na hivyo kusababisha magari kukosa mwelekeo kasha kupinduka.
KKatika ajali hiyo Zaidi ya watu kumi walijeruhiwa akiwemo dereva wa gari hilo Wasafiri Kibula ambao walikimbizwa katika kituo cha afya mtandika kwa ajili ya matibabu.
MWISHO.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>