
Akizungumza na wandishi wa habari jijini jana, Masaburi ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam alisema, kwenye katiba ya sasa inasema mamlaka hizo za serikali za mitaa zitajumuishwa kwenye nchi shirikishi ambazo ni Zanziba na Tanganyika ambayo haipo.
Alisema wanawataka wabunge kufanya hivyo kwa sababu muundo wakatiba hiyo haujakaa sawa, ambako pia lengo ni kutaka ALAT itambulike kwenye katiba kutokana na umuhimu wa wa mamlaka hiyo kwani imekuwa ikifanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi katika kila kona yanchi.
Masaburi alisema serikali za Mitaa zinadidimizwa kwa kutowekwa vizuri kuanzia kwenye katiba iliyopo sasa hadi Rasimu ya Katiba Mpya inayoendelea kujadiliwa mjini Dodoma kwani alisema kuwa Serikali za Mitaa ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi.
“Tunawaomba watanzania kutuunga mkono katika kupigia madaraka uwepo wa mamlaka ya serikali za mitaa kwani zimekuwa zikifanyakazi kila kona katika kuwaletea maendeleo,”
Masaburi alisema wanakusdia kwenda Dodoma kuwashawishi wajumbe wa Bunge la Katiba kuikataa rasimu hiyo, vinginevyo watapiga kelele kimataifa kuikataa Katiba Mpya kwa vile haitambui Serikali za Mitaa na watawashawishi wenyeviti, madiwani na watendaji kuanzia ngazi za vitongoji kuipinga rasimu hiyo ambayo hata kujadiliwa kwake wameshindwa kupata uwakilishi wa wajumbe wa Serikali za Mitaa.
Aidha ALATimepanga kukutana na waziri wa Tamisemi na mameya wa halmashauri zote nchini ili kuzungumzia kilio hicho cha miaka mingi cha kutothaminiwa na serikali.
“Serikali za Mitaa zimekuwa hazitambuliwi hata umoja wake kushindwa kupewa ruzuku ya kujiendesha tofauti na nchi nyingine, badala yake madiwani ambao hawana nafasi yoyote kiutendaji mara kwa mara kutuhumiwa kwa wizi, mtu ukimtuhumu mwizi wakati hajaiba na suala hilo likaendelea maana yake unamfundisha wizi,’’ alisema Masaburi.
Masaburi alisema msingi wa Serikali Kuu ni Serikali za Mitaa, hivyo inashangaza kuona zinaachwa kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.
Alisema kama wameona ni vizuri Serikali za Mitaa zikazungumzwa na nchi washiriki, basi hakuna budi kuirudisha rasimu hiyo, ili kwanza suala la Serikali mbili ama tatu likajadiliwa na kumalizika na ndiyo hatua ya pili ya kujadili Rasimu ya Katiba ikafanyika, vinginevyo watapiga kelele kuwa katiba hiyo imekosa mwelekeo wa demokrasia.