Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamuuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anaongoza kwa kupigiwa kura na wananchi kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.Akizungumza na Dira ya mtanzania Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era amesema zoezi hilo bado linaendelea na kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili kuend.elea kupiga kura kuchagua wahusika katika tamasha hilo.Mang’era alisema sambamba na wageni rasmi hao, mikoa inayoongoza kwa kupigiwa kura katika Tamasha la Pasaka ni Shinyanga, Dar es Salaam, Arusha na Ruvuma.Makamu Mwenyekiti huyo aliwataja Waimbaji wanaongoza kwa kupigiwa kura ni Christina Shusho, Edson Mwasabite, John Lisu pamoja na Rose Muhando.
Aidha Mang’era alifafanua kuwa ili kumchagua mgeni rasmi unaanza na neno Mgeni rasmi Pasaka unaacha nafasi kisha jina la mgeni rasmi kwenda 15327.
Mang’era alisema kumchagua mwimbaji katika tamasha hilo ni kuandika neno Mwimbaji Pasaka unaacha nafasi jina la mwimbaji kwenda namba 15327 sambamba na kuchagua mkoa, unaandika neno Mkoa Pasaka unaacha nafasi kwenda namba 15327.
Makamu huyo Mwenyekiti alitoa wito kwa Watanzania kupiga kura kuchagua nafasi hizo tatu ili kufanikisha tamasha hilo.