
Serekali imesema kuwa itafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa wale ambao wamehusika na tukio la ulipuaji wa bomu uliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni wa chadema watatiwa mbarano na kuchukuliwa
hatua kali za kisheria.
Hayo yamebainishwa na makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal wakati alipowatembelea wahanga wa bomu lililorushwa June 15 mwaka huu katika mkutano wa chadema.
Alisema kuwa serekali imepokea kwa masikitiko makubwa jambo hili ambalo ni la kigaidi na hatasita kumchukulia mtu yeyote aliyehusika na tukio hili hatua kali za kisheria iwapo atakamatwa.
Aliwataka wananchi wavute subira,wawe wastamilivu na pia wavumilivu haswa katika kipindi hichi ambacho upelelezi unaendelea na wasikate tamaa hata kama itachukuwa muda mrefu.
"Napenda kuwaambia msikate tamaa vuteni subra kwani aliyehusika atakamatwa tu hata kama ikitumia muda wa siku tatu ,siku kumi mwezi na hata miaka mitatu na zaidi lakini aliyefanya tukio hili atakamatwa tuata akienda wapi ninachopenda kuwaambia wananchi kuwa mjenge imani na serekali yanu ya jamuhuri ya muungano wa tanzania na mshirikiane nao na mwishowe matatizo haya yatakwisha"alisema Bilal
Aidha aliwataka wananchi wajenge imani na mapenzi mema na makubwa kwa nchi yao na hiyo tu ndo itawasaidia kuwavusha katika katika matatizo haya ambayo yanatokea kwa kwa kipindi hichi huku akiwasisitiza kuwa iwapo watajenga imani na mapenzi na serekali yao basi nchi yetu itakuwa na amani kama zamani na historia yake itaendelea kubaki kuwa Tanzania ni nchi ya amani. Chanzo: Mahmoud Ahmad Arusha