
Waziri waNchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Afya Juma Duni Haji nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

Muwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Thuwaiba Edington Kisasi wamwanzo kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir wa mwanzo kulia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

Muwakilishi wa Jimbo La Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu wakwanza kushoto wakibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haji Omar Kheir katikati na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Othman Masoud Othman katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.Picha na Yussuf Simai-Habari Maelezo-Zanzibar
----
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 17/06/2013
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeeleza kuwa kasoro zinazojitokeza katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapaswa kuingizwa na kujadiliwa katika mchakato wa Katiba unaoendelea.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Muhammed katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassour Juma aliyetaka kujua vigenzo vya uteuzi wa Waziri Mkuu unaofanywa na Rais na Zanzibar imetoa Mwaziri Wakuu wangapi tokea kuasisiwa Muungano.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo hadi sasa ndio inayotuongoza haikueleza vigezo vya uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania bali imetoa mamlaka ya uteuzi huo kwa Rais, na tangu kuasisiwa kwa Muungano hadi sasa Zanzibar imetoa Waziri mkuu mmoja ambae ni Salim Ahmed Salim.
Alifahamisha kuwa tangu kuasisiwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Zanzibar haijawahi kutoa Spika wala Naibu Spika isipokuwa imewahi kutoa Mwenyekiti wa Bunge Zubeir Ali Maulid katika kipindi cha mwaka 2005/2010.
Hata hivyo Waziri Aboud alisema kuwa nafasi bado ipo ya kuweza kueleza kero zilizopo ambazo zinaonekana kwamba ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania.
Alikiri kuwa ipo hati ya makubaliano na maridhiano ya kikatiba kwa nchi zote mbili zilizokuwa huru na mamlaka yake kamili na pia si kweli kuwa Zanzibar haina wasomi .
Waziri alieleza kuwa kero za Muungano bado zipo na ndio sababu moja wapo ya kuanzisha mchakato wa katiba ili kuzitafutia ufumbuzi kero hizo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema kuwa wanavyojuwa ni kua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja kero zilizozopo zinafanywa kwa makusudi